Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea na ushahidi wa upande wa utetezi dhidi ya kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji kwa kuwa Hakimu anayeendesha kesi hiyo anamajukumu mengine ya kiofisi.

Kutokana na hayo, kesi hiyo sasa itasikilizwa kwa siku tatu mfulukizo, Septemba 25, 26, na 27 ambapo mashahidi wa utetezi watafika kutoa ushahidi wao kwa kuanza na Manji. Wakili wa Serikali Mwandamizi Timon Vitalis ameileza mahakama kuwa, kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikiliza shahidi wa upande wa utetezi ambapo Manji mwenyewe alitakiwa kuanza kujitetea lakini kutokana na kuchelewa kuanza asingeweza kuendelea kwa kuwa anasafiri kikazi.

Hakimu Cyprian Mkeha alimuuliza Manji kwa nini alichelewa kufika na hali alitakiwa kufika asubuhi ya saa tatu, alisema kuwa aliambiwa na wakili wake kuwa Hakimu ameenda kwenye kikao Mahakama kuu na hakujua kama amerudi mapema.

"Samahani mheshimiwa niliambiwa haupo, nikadhani haujarudi, samahani sana Mheshimiwa" amesema Manji.

"Ni kweli, nilienda kwenye kikao Mahakama kuu lakini nilirudi mapema na sasa natakiwa kwenda tena huko" amesema Mkeha.
 Yusuf Manji akiwasili Mahakani hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.
Yusuf Manji azungumza na Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub nje ya Mahakama ya Hakumu Mkazi Kisutu, Mchana huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...