Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu, (wapili kulia), akifurahia jambo na wahandisi na mafundi
wa TANESCO alipotembela mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20,
2017.
Naibu Waziri, Mhe. Subira Mgalu(katikati), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANSECO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka,
(kulia), na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (anayeshughulikia
usafirishaji umeme), Mhandisi Kahitwa Bishaija, (kushoto), wakiwasili
kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kigamboni
jijini Dar es Salaam Oktoba 20, 2017.
Wahandisi wa TANESCO wakimalizia
kazi ya kufunga mitambo kwenye kituo cha Kigamboni.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa
Nishati, Mhe. Subira
Mgalu ameendelea na ziara yake ya kujifunza kwa kukagua miradi mingine miwili
mmoja wa ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme Kimbiji na kingine cha kupoza
umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2017.
Alhamisi Oktoba
19, 2017, Mhe. Mgalu
alifanya ziara kama hiyo kwa kutembelea vituo viwili vya kupoza umeme vya
Mbagala na Kurasini wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiwa Kigamboni, Naibu
waziri ambaye alifuatana na Katibu Tawala wa Wilaya mpya ya Kigamboni,
Bi. Rachel
Mhando na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na viongozi
wengine wa juu wa Shirika hilo, alianza kwa kukagua kituo cha Kigamboni ambapo
aliwakuta mafundi wa TANESCO wakimalizia kufunga mitambo kwenye kituo
hicho.
Aidha Naibu waziri
alimalizia ziara
yake kwa kutembelea eneo la ujenzi wa kituo kipya cha Kimbiji ambapo kazi ya
kusafisha eneo la ujenzi nayo imekamilika na kinachosubiriwa ni kuwasili kwa
vifaa ili ujenzi uanze.
Mheshimiwa Mgalu
alisema kutokana na
ongezeko kubwa la watumiaji wa umeme, vituo hivyo vitasaidia sana kuboresha
huduma ya upatikanaji umeme hususan katika kipindi hiki ambacho serikali ya
awamu ya tano imejielekeza kujenga uchumi wa viwanda na hitajio kubwa katika
utekelezaji wa mpango huo ni upatikanaji wa umeme wa uhakika.
“Niwashukuru tu
kwa ksuema, ziara
yangu hii ni ya kwanza kwenye eneo hiki tangu niteuliwe na nimeona nije ili
nijionee jitihada hizi za kuboresha hali ya umeme wilayani Kigamboni ambapo
kuna uhitaji mkubwa wa umeme ,kutokana na ongezeko kubwa la watu.”
Alisema.
Akieleza zaidi
Mheshimiwa Mgalu
alihimiza Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ambalo kwa niaba ya serikali ndilo
linatekeleza mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi ili hatimaye wananchi wapate
huduma ya umeme katika hali bora zaidi.
Aidha Katibu
Tawala wa Wilaya ya
Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, Aliishukuru serikali kwa kuleta mradi huo katika
wilaya hiyo na kusema serikali wilayani Kigamboni itatoa kila aina ya msada ili
kuhakikisha mradi huo mkubwa unakamilika.
“Hii ni wilaya
mpya ni jambo la
kushukuru kuwa katika kipindi kifupi wilaya inaletewa mradi mpya wa kuboresha
umeme kwa kweli wananchi wana matarajio makubwa na mradi huu na sisi
tumefarijika sana.” Alisema Katibu Tawala wa wilaya ya Kigamboni.
Naibu waziri akipatiwa maelezo
na Naibu Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi
Kahitwa Bishaija, (wapili kushoto). Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...