THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SAROTA AWAASA WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA STAMICO KUKUZA UBUNIFU

Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi John Nayopa leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi John Nayopa (wa nne kutoka kulia waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi walioshiriki katika kikao cha tatu cha Baraza hilo kilichomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa STAMICO Bwana Lameck Kabeho akitoa nasaha za utangulizi na utambulisho katika mkutano wa 3 wa Baraza hilo uliofanyika hivi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa STAMICO Makao Makuu Dar es Salaam na wale wa kutoka Dodoma, wakiwa ndani ya ukumbi wa mikutano wa Shirika hilo,  kushiriki katika mkutano wa tatu wa Baraza, tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo Februari, 2017.

KAMISHNA Msaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Madini Bw. Julius Sarota amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kukuza ubunifu katika kutekeleza majumu yao ili kuleta ustawi endelevu wa Shirika hilo na tija kwa Taifa.

Bw. Sarota ametoa rai hiyo leo, wakati akizungumza katika mkutano wa tatu wa Baraza la Wafanyazi wa STAMICO, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini; uliofanyika katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Bw. Sarota amesema Baraza la Wafanyakazi mahala pa kazi ni chombo muhimu cha kukuza ustawi wa taasisi husika; hivyo ni wajibu wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la STAMICO kuongeza ubunifu na kutekeleza miradi ya utafiti na uchimbaji madini; itakayoleta faida kwa STAMICO na kukuza uchumi wa Tanzania.

“ Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza azma ya Taifa ya kujenga Tanzania ya Viwanda, ambavyo vitahitaji madini kutumika kama mali ghafi. Nichukue fursa hii kusisitiza STAMICO mtekeleze miradi ya uchimbaji madini itakayosaidia kutoa mali ghafi kwa viwanda vinavyotarajiwa kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini.” Alisisitiza Bw. Sarota.

Amesema STAMICO inabidi iongeze mwendo katika utekelezaji wa miradi yake ya vipaumbele, ili kwenda sambamba na kasi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi na ya viwanda; hatimaye kumudu soko la mali ghafi za madini nchini kama vile phosphate na graphite, hatua ambayo itasaidia kuwazuia wenye viwanda kuhangaika kuagiza mali ghafi hizo kutoka nchi za nje.

Kusoma zaidi bofya hapa.