Afisa Muuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Vedastus na Arianna Minghetti wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimnywesha maziwa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo bila ya kufungua kifua (Catheterization) katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.
Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kufungua kifua na kuziba tundu la moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la Meding Kids la nchini marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) na kuzibua mishipa ya Moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
Maafisa Uuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwezao wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakijadiliana kuhusu maendeleo ya wagonjwa waliolazwa katika chumba hicho baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.Picha na JKCI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...