KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waumini wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange, Miono,  Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.
Zulia pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani.
Mara baada ya kukabidhi Zulia na fedha hizo, Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.
Akiungumza mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba ya waumini wa Msikiti huo wanamshukuru Mhe. Rais kwa kuitikia ombi lao la kupata zulia, na kwamba  kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe. Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.
Sheikh Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea  kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchini kuungana nao kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pwani
17 Novemba 2017.
Msaidizi wa Rais Kanali Msafiri Mkeremy akimkabidhi Imamu wa Msikiti wa Noor kijijini Mkange, Miono, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani Sheikh Khamis Nassor wakati alipowasilisha msaada wa zulia la kuswalia msikitini hapo akiwa kaongozana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Jaffary Haniu (nyuma ya Imamu) Ijumaa Novemba 17, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...