Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bregedia John Mbungo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu atakayewezesha kupatikana  kwa aliyekuwa mhasibu wa taasisi hiyo, Godffrey Gugai anayedaiwa kujilimbikizia mali.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bregedia John Mbungo akionesha picha ya aliyekuwa mhasibu wa taasisi hiyo, Godffrey Gugai  kwa waandishi wa habari leo JIjini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko
Taasisi ya kuzuia na kupamabana na rushwa nchini (TAKUKURU) imetengaza zawadi nono ya shilingi milioni kumi kwa mtu atayewezesha kupatikana kwa aliyekuwa mhasibu wa taasisi hiyo, Godffrey Gugai anayedai kuwa na ukwasi mkubwa wa fedha na mali isiyolingana na kipato chake halali akiwa kama mtumishi wa umma.
 Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bregedia John Mbungo amesema, baada ya kuchunguza na kutoa taarifa ya awali walimuita Gugai na kumuhoji ambapo alionyesha ushirikiano wa kujibu hoja hizo zinazomkabili na kuwa na mali nyingi kuliko kipato chake
Amesema, kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha sheria ya Kuzuia na kupaambana na Rushwa ni kosa la jinai kwa afisa wa serikali au mtumishi wa umma kuwa na mali nyingi au maisha ambayo yanazidi kipato chake bila ya kuwa na maelezo yoyote anayoelezea mali zile amezipata wapi au kwa namna gani.
“Bwana Gugai aliweza kujikusanyia mali nyingi ambazo awali tulijaribu kumuuliza na alielekea kuonyesha ushirikiano lakini baadae alipoona kwamba hana maelezo ya namna gani amezipata zile mali akapotea. tumeendelea kumtafuta na taarifa ambazo tumekuwa tukizipata amekuwa ni mtoro amekimbilia nje ya nchi kupitia njia ambazo siyo rasmi” amesema Bregedia Jenerali Mbungo.
Mhasibu huyo anamiliki maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano na pikipiki pamoja na viwanja 37.
 Amesema ni kosa kubwa kwa mtumishi wa umma kutumia ofisi yake kujipatia mali  nje ya kipato akipatacho ni kosa, aliwahi kuchukuliwa maelezo, alipogundua hana maelezo sahihi akaamua kukimbia.
Maghorofa, nyumba za kawaida na viwanja vya mhasibu huyo viko kwa mtawanyiko katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya ghali karibu na bahari, Kigamboni na Mbweni jijini Dar es Salaam na pia Bagamoyo mkoani Pwani. Kwingineko kuliko na mali hizo ni Kinondoni (Dar), Musoma, Nyegezi, Kiseke jijini Mwanza, Arusha na Tanga
Hata hivyo, mali za Gugai zimewekewa zuio la mahakama na mawakala wake na watu wengine wote wanaomwakilisha wamezuiwa kuuza au kuhamisha umiliki au kuweka dhamana mali zote zilizowekewa zuio.

 Pia Msajili Msaidizi wa magari ameagizwa asiruhusu uhamishaji wa umiliki wa vyombo vya moto vilivyowekewa zuio mpaka mahakama itakapoelekeza vinginevyo.
mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...