NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
WATANZANIA wanatakiwa kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kupata vipimo kutoka kwa wataalam kabla ya kutumia dawa kwa mazoea ili kuepuka usugu wa vimelea vya wagonjwa kwenye miili yao na kusababisha vifo vya mara kwa mara.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mradi wa kupambana na usugu wa vimelea kutoka Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) Dkt. Raphael Sallu wakati wa semina na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tatizo la kutumia vijiuasumu(Antibiotics) bila ya kupata vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya limekua kubwa ambalo linasababisha madhara ya kiuchumi na uhai kutokana na kuzidiwa na vimelea vya ugonjwa ambavyo vinakua sugu kutokana na matumizi mabaya ya dawa hapa nchini” alisema Dkt. Sallu.

Aidha, Dkt. Sallu amesema kuwa elimu ya kutumia dawa bila ya kupata ushauri na vipimo kutoka kwa wataalamu wa afya ianze kutolewa kuanzia ngazi za shule ya msingi na ngazi ya jamii kwa ujumla.

Mbali na hayo Dkt. Sallu amesisitiza kuwa wanahabari wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuelimisha umma umuhimu wa kutumia dawa kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalam kuhusu ugonjwa unaomsumbua pamoja na matibabu yake.
Mwakilishi Mkuu wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea (FAO) Dkt. Raphael Sallu akiwasilisha mchango wake wakati wa semina na Waandishi wa habari kuhusu matumizi bora ya Antibiotic, ilofanyika katika ofisi za FAO jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Taifa wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea katika Shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) Dkt. Bachana Rubegwa (aliesimama) akieleza maudhui ya semina hiyo niliyofanyika mapema leo katika ofisi za FAO jijini Dar es Salaam.

 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa kupambana na usugu wa vimelea vya ugonjwa Bi Rose Shija akiwasilisha mchango mbele ya wadau wa habari, pembeni yake ni Afisa Habari wa Wizara ya Afya Catherine Sungura.
 Mmoja ya wadau wa Habari ambae pia ni mmiliki wa Blog ya Full Shangwe akitoa mchango mbele ya wadau wenzie wa habari na wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa katika Semina ya kuhamasisha matumizi bora ya antibiotic.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...