Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo ametilia shaka makusanyo
katika hospitali ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kuagiza
kusimamiwa vyema ukusanyaji mapato.
Jafo
ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ndani ya Halmashauri ya
wilaya hiyo ambapo alisema amegundua kuna kila dalili kwamba mapato ya
hospitali hiyo yanavuja kutokana na taarifa nyingi za fedha za Malipo ya
wagonjwa kutoingizwa kwenye mfumo wa kielekroniki hivyo kusababisha
kukusanya wastani wa Sh.milioni 4 kwa mwezi.
Katika
ziara hiyo, Jafo amezungumza na watumishi wa Halmashauri ya Misungwi
ambapo amewasisitiza watumishi na viongozi kuwa na mahusiano mema ili
waweze kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.Jafo amesisitiza kwamba kila mmoja anapasa kumthamini mwenzake na kushirikiana katika kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha
Jafo amewapongeza walimu wa shule ya sekondari Misasi kwa kufanya vyema
sana kwani wamefanikiwa kupeleka watoto 45 kidato cha tano kati ya
wanafunzi 100 waliomaliza kudato cha nne mwaka jana.
Baada ya ziara hiyo waziri Jafo ameendelea na ziara yake wilayani sengerema mkoani Mwanza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua hospitali ya wilaya ya Misungwi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata taarifa ya miradi ya elimu kutoka kwa viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa maabara katika sekondari ya Misasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...