Rais wa Palestina Mheshimiwa Mahmuud Abbas

Na Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania)
Mkutano wa dharura wa Kiislamu umefanyika mjini Stambul-Uturuki, kujadili azimio la Rais wa Marekani Donald Trump la kuitambua Jerusalem kuwa ni mji mkuu wa Israeli.  Katika hotuba ya Rais wa Palestina Mheshimiwa “Mahmuud Abbas”,  ametahadharisha ya kwamba  hakuna amani  wala utulivu utakayopatikana katika eneo la mashariki ya kati bila ya kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa dola ya Palestina.
Aidha, Rais Abbas  amelielezea  azimio la Trump kuwa ni uhalifu mkubwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kimataifa na mikataba iliyosainiwa, huku akilizingatia azimio hilo kuwa ni sawa na lile “Azimio la pili la Balfour”. 
Rais Abbas ameweka wazi kwamb,  Marekani  imeshusha ustahiki wake katika mchakato wa kisiasa kwa sababu ya kupendelea kwake kote kwa  Israeli, huku akiashiria kwamba azimio la Trump halitoipa Israeli uhalali wowote mjini Jerusalem.
Rais Abbas ametoa wito kwa Mkutano huo, kufafanua uhusiano wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu “OIC” na nchi nyingine duniani,  kuhusiana na nafasi yake juu ya maazimio ya Trump. Rais Abbas pia ametaka kuchukuliwa maazimio yanayoilazimisha Israeli kutekeleza  maazimio ya kimataifa kuhusu Palestina, huku akiitaka dunia Kuangalia upya kuitambua kwake Israeli, muda wa kuwa inaendelea kukiuka sheria za kimataifa.
Rais wa Palestina ameshukuru misimamo ya awali ya Chuo Kikuu Kitukufu Cha Azhar na Papa Francis kuhusu Jerusalem,kama alivyowashukuru wananchi wake wakiwemo wakristo na waislamuwalio ndani na nje  ya mji wa Jerusalem, ambao ndio wanaoutetea Msikiti wa Aqsana Kanisa la Ufufuo: “Ninawaambia kwamba, hakika sisi tutaendelea kuwa pamoja na tukiwa sawa katika kuitetea Jerusalem, huku tukiwa tumethibiti kukabili njama ambazo zinalenga mji wetu na mji mkuu wetu,hadi tupate uhuru wetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...