Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
akimvisha medali golikipa wa timu ya mpira wa miguu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar
Ahmad Suleiman wakati wa kufunga fainali za Michezo ya Vyuo Vikuu iliyofanyika
Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017. Chuo Kikuu cha
Zanzibar waliibuka washindi wa mpira wa
miguu kwa wanaume.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania (OUT) wakati wa kufunga fainali za Michezo ya Vyuo Vikuu iliyofanyika
Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017. OUT waliibuka
washindi wa mchezo wa kikapu kwa wanaume dhidi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na washiriki wa Michizo ya
Vyuo Vikuu (Hawapo Pichani) wakati akifunga fainali za Michezo hiyo
iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017.
Waliokaa kulia kwake wa kwanza ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe.
Antony Mavunde,Wa pili ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Idris
Kikula na Mtangazaji wa Clouds Fm Ndg. Shafii Dauda.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijiandaa
kufunga kikapu wakati wakufunga Michezo ya Vyuo Vikuu kwenye Mchezo wa Fainali
ya mpira wa kikapu kati ya timu ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Tanzania (OUT) na
Chuo Kikuu cha Dododma (UDOM) iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma
leo Tarehe 20/12/2017, wa Pili kushoto ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana
Mhe. Antony Mavunde. OUT waliibuka washindi wa mchezo wa kikapu kwa wanaume. PICHA NA:OCTAVIAN KIMARIO-WHUSM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...