MTANDAO
wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikiana na African Population and
Health Research Center (APHRC) umekutana na wadau wa elimu jijini Dar es
Salaam kujadili namna ya kutekeleza mradi wa kusaidia maboresho ya
elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza
katika kikao hicho cha majadiliano kilichoshirikisha viongozi kama
wabunge, madiwani wa maeneo hayo pamoja na watendaji wa sekta ya elimu,
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao
alisema kikao hicho kinajadiliana namna ya kutekeleza mradi huo utakao
lenga kuboresha elimu.
Akifafanua
zaidi, Bi. Sekwao alisema kikao hicho kitaangalia matatizo gani kielimu
yanayowakwaza watoto wanaoishi katika miji na majiji yenye msongamano
wa makazi kiujumla na kuangalia namna wanaweza kukabiliana nayo. Alisema
mradi huo utakuwa wa miaka miwili lakini baadaye unaweza kuwa endelevu
kadri ya mahitaji yake kwa jamii husika.
Akichangia
katika kikao hicho, Mthibiti Ubora wa Shule Wilaya za Temeke na
Kigamboni, Mashaka Munjalloh alisema mradi huo utawasaidia watoto kutoka
maeneo yenye msongamano kupata elimu bora itakaowasaidia katika maisha
yao.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao akizungumza kufungua katika kikao cha wadau wa elimu jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kutekeleza mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Mtafiti Mwandamizi na Kiongozi wa Kitengo cha Elimu na Uwezeshaji Vijana wa African Population and Health Research Center (APHRC) Moses Ngware akiwasilisha mada katika kikao cha wadau wa elimu jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kutekeleza mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.
Wapili kulia ni Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia akichangia mada katika kikao cha wadau wa elimu jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kutekeleza mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (katikati) akichangia mada katika kikao cha wadau wa elimu jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kutekeleza mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (kushoto) wakiwa katika kikao hicho.Washiriki katika kikao cha wadau wa elimu jijini Dar es Salaam wakiwa katika kikao kujadili namna ya kutekeleza mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...