THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAKAZI DODOMA WALAMBA MILIONI 1 KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MTAA WAO


NA RAMADHANI JUMA,OFISI YA MKURUGENZI, MANISPAA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge ameahidi kutoa motisha ya Shilingi 1,000,000 kwa wakazi wa mtaa wa Zahati uliopo Kata ya Kikuyu Kaskazini katika Manispaa ya Dodoma kufuatia wakazi hao kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa Mazingira unaofanyika kila Jumamosi katika Manispaa hiyo.

Mheshimiwa Mahenge alitoa ahadi hiyo wakati alipowaongoza wakazi hao katika zoezi la usafi wa Mazingira katika Mtaa huo mwishoni mwa wiki, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kufanya usafi wa Mazingira kila Jumamosi aliyoianzisha yeye mara tu baada ya kuhamishiwa Mkoa humo, kwa lengo la kuuweka Mji Mkuu wa Nchi katika hali ya usafi wakati wote.

Alisema fedha atakazowapa wakazi wa Mtaa huo ni motisha na kuwaunga mkono kwa juhudi walizoonesha na kwamba zitawasaidia katika kuboresha hali ya usafi katika eneo lao kwa kununua vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi.

Alisema amefurahishwa na namna wakazi wa Mtaa wa Zahati walivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo na kutoa wito kwa wakazi wa maeneo mengine katika Manispaa kuiga mfano huo ili kwa pamoja waweze kuufanya Mji wa Dodoma kuwa namba moja kwa usafi wa Mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge (kulia) alipowaongoza wakazi wa Mtaa wa Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini (pichani nyuma) kufanya usafi wa Mazaingira kila Jumamosi kufuatia Kampeni ya Usafi wa Mji aliyeianzisha yeye. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi.
Wakazi wa Mtaa wa Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini Manispaa ya Dodoma wakifanya usafi wa Mazaingira wa kila Jumamosi kufuatia kampeni ya Usafi wa Mji iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Dokta Binilith Mahenge.
Zoezi la usafi likiendelea katika Mtaa za Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge (kuli) akisikiliza kero mbalimbali za Wananchi wa Mtaa wa Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini Manispaa ya Dodoma baada ya zoezi la usafi wa Mazingira wa kila Jumamosi. Mkuu huyo wa Mkoa amejiwekea utaratibi wa kusikiliza kero za wakazi wa Mtaa husika baada ya kufanya nao usafi wa Mazingira.PICHA: RAMADHANI JUMA-OFISI YA MKURUGENZI MANISPAA YA DODOMA.