Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kibengu wametumia jumla ya shilingi milioni mia moja kumi na tisa na laki mbili (119,200,000) katika ujenzi wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kijiji hicho lengo likiwa katika kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.
Akizungumza na wananchi katika kijiji hicho mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.
“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa
Mgimwa alieleza kuwa pesa hiyo itatumika katika maeneo yafuatayo ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Kibengu utatumia gharama ya shilingi milioni thelathini (30,000,000) hadi kukamilika kwake,kuingiza umeme zahanati na kwenye nyumba za waganga imegarimu kiasi cha shilingi 1,200,000/=,ujimbaji wa kisima shilingi 2,00,000/=,ujenzi wa nyumba za walimu mbili kwa moja itagharimu kiasi cha shilingi 25,000,000/= na shule ya msingi Kibengu kutafanyika ujenzi wa madarasa matatu ambayo yatagharimu kiasi cha shilingi 21,000,000/=.
Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akitoa mfano wa kufanya kazi kwenye ujenzi wa vyumba vitatu vya shule ya msingi Kibengu ambako nako wananchi wamechangia nguvu zao
Katibu wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Mufindi akiwa na katibu wa mbunge idara ya uhamasishaji na michezo Lwimbo nao wakijumika na wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Kibengu
Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi katika eneo ambalo vyumba vitatu vya madarasa vinajengwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...