Ratiba ya mazishi ya mama yetu mpendwa Peres Kingunge Ngombale Mwiru(Mama Kinje)
Jumatano tarehe 10/1/2018
- Saa 10:00 jioni mwili kutoka Hospitali kuelekea nyumbani Victoria/Makumbusho Kingunge street.
-Saa 11:00 jioni mwili kuwasili nyumbani na taratibu za ibada mila na desturi kuendelea usiku mzima(mkesha)
******************************
Alhamisi tarehe 11/1/2018
-Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
-Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote
-Saa  4:00  asubuhi mpaka saa 7:00 mchana kuaga mwili wa marehemu(waombolezaji wote)
-Saa 7:15 mchana mwili kuelekea kanisa la St. Peter’s Oysterbay Kwa ibada(waombolezaji wote)
-Saa 7:30 mchana -8:30 mchana ibada ya kumuombea marehemu
-Saa 8:30 mchana mpaka 9:30 mchana  kuaga mwili wa marehemu Kanisani.
-Saa 9:45 mwili kuelekea makaburini Kinondoni.
-Saa 10:00 jioni 12:00 jioni shughuli  za mazishi( waombolezaji wote)
-Saa 12:00 - waombolezaji wote kuelekea nyumbani Kwa Mzee Kingunge victoria.
-Saa 1:00 usiku - saa 2:30 usiku kupata 
chakula cha jioni Kwa waombolezaji wote.

Tunawashukuru sana Kwa ushiriki wenu wa 
Hali na mali katika wakati huu mgumu
Mungu awazidishie sana.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe🙏
Omary A. Kimbau( msemaji wa familia)

 Kinjeketile Ngombale Mwiru (kushoto) akiongea na marafiki waliofika kumfariji kufuatia kifo cha mama yake. Chini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg. Kheri Denis James akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo alipofika nyumbani kwa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru jijini Dar es salaam kutoa rambirambi zake. 
Mazishi ya mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Marehemu Peras Kingunge, yamepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Janury 11, 2018 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, msemaji wa familia Bw. Omari Kimbau ametangaza. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...