Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametoa onyo kali kwa viongozi wa kisiasa wa Wilaya ya Kiteto kuwa atawachukulia hatua kali wote watakaosababisha migogoro ya ardhi kwa wananchi. 

Akizungumza kwenye kata ya Njoro, Mnyeti alisema atawachukulia hatua kali wanasiasa hao kwani yeye siyo mkuu wa mkoa wa maboksi anayeogopa kulowanishwa na mvua. Alisema alipata taarifa ya baadhi ya wanasiasa wanaotumia migogoro ya ardhi kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa, ila hatawafumbia macho wanasiasa wa aina hiyo waliopo wilayani Kiteto. 

"Tumekuwa na migogoro isiyokwisha, wewe una shamba lako kwenye kijiji cha Bwawani kuna mtu anakuzuia kulima hapa Njoro? au ukiishi hapa Njoro kuna mtu amekunyima kununua nyumba kule Kibaya makao makuu ya wilaya?" alihoji Mnyeti. Alisema atawashughulikia wanasiasa hao wanachochea migogoro ya ardhi baina ya watu na watu na kijiji na kijiji ili iwe funzo kwao na hawatasahau kitendo hicho. 

"Wanasiasa hao wababaishaji, wanaojaribu kuishika serikali sharubu nitakula nao sahani moja, kwani hatuwezi kukubali hali hiyo ijitokeze na kuacha kuchukua hatua kwao bila kuangalia vyeo vyao," alisema Mnyeti. Hata hivyo, alimuagiza mkuu wa wilaya ya Kiteto, mhandisi Tumaini Magessa kuhakikisha vijiji vyote vinawekewa alama za mipaka ili kuondokana na migogoro ya ardhi. 
 Wananchi wa Kata ya Njoro Wilayani Kiteto, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza nao,  juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akizungumza kwenye Kata ya Njoro Wilayani Kiteto juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi, kushoto ni mbunge wa jimbo hilo Emmanuel Papian na Mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Tumaini Magessa.
Wananchi wa Kata ya Njoro Wilayani Kiteto, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza nao,  juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...