Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SERIKALI imetoa tamko kuhusu ushiriki wa mwanariadha Alphonce Simbu katika mashindani ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika April mwaka huu.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Gold Coast nchini Australia, ambapo Serikali na Kamati ya Olimpiki Taifa (TOC) walipokea barua kutoka kwa Simbu ya kuomba ashiriki mashindano ya London Marathon ambayo ni makubwa zaidi kuliko ya Jumuiya ya Madola.
 
Simbu ambaye ni mshindi wa tatu wa London Marathon 2017, Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Riadha (RT) na kamati ya Olimpiki (TOC) walikaa katika kikao cha pamoja Januari 13 mwaka huu na waliridhia ombi la Simbu kuweza kushiriki huko na pia aweze kupata muda wa kujiandaa zaidi ili kuiwakilisha vyema Taifa katika mashindano hayo.

Akitolea ufafanuzi huo, Ofisa habari wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Najaha Bakari amesema kuwa Watanzania wasiwe na hofu kwani wameshafanya uchaguzi wa wawakilishi wa kwenda kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola na wanaamini kuwa watafanya vizuri zaidi na kurudisha medali nyumbani.

Mbali na hilo, Najaha amesema kuwa vyama vyote vya michezo nchini vilivyopo chini ya BMT wanatakiwa kuwasilisha kalenda za mwaka kabla ya Februari 10 mwaka huu na kwa chama chochote ambapo hakitafanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Kuna vyama kila mwaka vinakuwa haviwasilishi kalenda yao ya mwaka ambapo mfano wake ni Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) ambao wao wanaona ni chama kikubwa sana ila wanatakiwa wajue kuwa wote ni wadogo na wanatakiwa wawasilishe kalenda yao BMT,"amesema Najaha.

Najaha amesisitiza kuwasilishwa kwa kalenda hizo kutasaidia katika kuandaa miundombinu ya viwanja kwani kumekuwa na muingiliano wa baadhi ya matukio ya michezo kutokana na kutokuwa na kalenda za vyama vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...