Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMPUNI  ya Kimataifa ya Kohler ya bidhaa bora za ujenzi imefungua duka la kusambaza bidhaa  zake katika Kampuni ya ABC Emproria jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Kampuni hiyo Kanda ya Bara ya Kusini Asia na EMEA, Salil Sadanandan amesema kampuni imeamua kuingia katika soko la Tanzania kutokana na kufanya utafiti na kubaini kuwa ni moja ya nchi katika ukanda wa Afrika Mashariki sekta ya ujenzi inakuwa kwa kasi.

“Kutokana na kasi ya kukua kwa sekta ya ujenzi nchini tumeona kuna umuhimu wa kusogeza huduma ya upatikanaji wa bidhaa za Kohler kwa urahisi wakala wetu wa ABC  Emporio ambayo ina uzoefu mkubwa wa kuuza na kufunga vifaa vya ujenzi , huu ni mwendelezo wa kupanua masoko yetu barani Afrika ambao tayari wana matawi katika nchi za Kenya na Uganda” Amesema Sadanandan .

Nae Rais wa Kampuni  ya ABC Emporio, Muhamed Hadani amesema kuwa wanajivunia kuwa mawakala wa kuuza bidhaa za Kohler pia ni fursa pekee kwa watanzania kupata bidhaa hizo kwa gharama nafuu
 Rais wa Kampuni ya Kohler Kanda ya Bara ya Kusini Asia na EMEA, Salil Sadanandan akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ufunguaji wa duka la vifaa vya ujenzi leo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Kampuni  ya ABC Emporio, Muhamed Hadani akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na usambazaji wa bidhaa za Kohler leo jijini Dar es Salaam.
 Msemaji wa Kampuni ya ABC Emporio, Matha Majura akizungumza na wandishi wa habari  kuhusiana na kampuni huyo inavyofanya kazi hapa nchini.
Muonekano wa duka la vifaa vya ujenzi lililofunguliwa leo jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...