THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

IDARA YA UHAMIAJI WAFANYA USAFI KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM, SHULE YA MSINGI MATUMAINI


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

IDARA ya Uhamiaji nchini imefanya usafi katika Kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu na Shule ya Msingi ya Matumaini ya Jeshi la Waokovu ‘Salvation Army’ iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kufanya usafi katika shule hiyo,kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Idara hiyo , Kamishina wa Utawala na Fedha, Edward Chogera amesema tangu kutangzwa Siku ya Jumamosi ni ya kufanya usafi Idara yai imekuwa ikifanya jitihada za kufanya usafi huo katika maeneo ambayo yana mchango kwa jamii.

Amesema shule ya Matumaini na kituo ni sehemu muhimu kutokana na watoto wanaosoma hapo kuwa na mahitaji maalumu.Kituo hicho hakiwezi kufanya chenyewe kutokana na mazingira ya watoto hao.Ameongeza mbali ya kufanya usafi katika kituo hicho wametoa pia msaada wenye thamani sh.500,000 ambao umetokana na wafanyakazi wa idara na wadau wenye ni njema kusaidia kundi maalumu ya kituo cha Jeshi la Uokovu .

Aidha amesema katika kipindi kijacho wamepanga kuwafikia watu wengine katika kufanya usafi ikiwa ni sehemu ya wafanyakazi kujua jamii inayowazunguka.Msaada waliotoa ni , Mchele, Maharage sukari , Mafuta ya kula , Sabuni za kuogea , Unga wa mahindi na mafuta ya kupakaa kwa wanafunzi wenye Ualbino .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho,Timoth Sinana amesema licha kupata elimu,watoto wamekuwa wamekuwa wakiendelezwa kwenye mambo mbalimbali yakiwamo ufundi nguo na kuendeleza vipaji vyao.Amesema wanafunzi hao wamekuwa bora kimkoa katika suala la vipaji.
Kamishina wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji , Edward Chogera akizungumza wanafunzi na walimu pamoja na walezi wa kituo na shule ya Matumaini ya Jeshi la Waokovu Salvation Army mara baada ya kumaliza usafi katika kituo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Jeshi la Waokovu pamoja shule ya Matumaini, Timoth Sinana akizungumza kuhusiana na historia ya shule hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1969 pamoja na mafanikio ya shule hiyo .
Msaada uliotolewa katika kituoa hicho ni , Mchele, Maharage sukari , Mafuta ya Kula , Sabuni za Kuogea , Unga wa Mahindi pamoja na mafuta ya kupakaa kwa wanafunzi Wenye Ualbino .  

Baadhi wa wafanyakazi katika shule ya msingi ya matumaini na kituo cha jeshi la Waokovu