THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MWIJAGE MGENI RASMI KONGAMANO LA VIWANDA KESHO UKUMBI WA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM


Na Humphrey Shao, Globu Ya jamii 
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kufungua kongamano kuhusu Maendeleo ya Viwanda Tanzania litakalo fanyika katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere February 23 Mwaka huu. 
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Afisa Habari wa chuo Hicho Evelyn Mpasha amesema kuwa Kongamano hilo kubwa litawaleta karibu wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo ya Viwanda nchini. 
 “Kongamano hili litaangazia Masuala ya Maendeleo ya Uchumi , Uwekezaji Endelevu katika Viwanda, Ujasiliamali katika Uwekezaji katika Viwanda kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na sekta binafsi” amesema Mpasha. 
 Kwa upoande mmoja wa watoa mada katika kongamano hilo Binto Mawazo amesema kongamano hili ni sehemu ya juhudi za chuo kushiriki katika kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuipeleka Tanzania katika uchumi wa Viwanda . 
 Binto amesema kuwa MNMA kama chuo ni wadau Muhimu sana katika kukiwezesha wananchi kufika malengo ya Rais kuipeleka nchi katika uchumi wa kati.