MBUNGE wa jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,Mary Michael Nagu amesema kuanzishwa kwa mfuko wa maji unaotokana na fedha zinazopatikana kwenye mauzo ya mafuta ya vyombo vya moto utakuwa sukuhisho la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwenye maeneo mengi ya vijijini.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Diyagwa baada ya kupokelewa na wananchi wa Kijiji hicho waliokuwa wakipeperusha bendera ya CCM huku wakiwasilisha kilio chao cha maji,Mbunge huyo alisema moja ya changamoto inayowasumbua wananchi wa Hanang ni tatizo la huduama ya upatikanaji wa maji safi na salama.
“Tena niwaambie ni miaka na Tanzania kama kuna shida ni maji na bila maji hakuna maendeleo,sisi hapa tumshukuru mungu nilikaa huko serikalini tukasemaa bila kuunda mfuko wa maji,maji Tanzania hayatakuwa”alisisitiza Mbunge huyo.
Aidha Mbunge huyo hata hivyo aliweka bayana pia kwamba baada ya serikali kulitambua tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji  imeshaunda mfuko huo ambao fedha zake zinapatikana kwa njia ya kununua mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa kila shilingi 50 huingia kwenye mfuko huo.
Kwa mujibu wa Nagu idadi kubwa ya miradi ya maji inakwamishwa na wakandarasi wasiokuwa na uwezzo wa kifedha za kukamilisha kwa wakati kazi walizokabibidhiwa,ambapo hata hivyo alionekana kukerwa na mamlaka zenye dhamana ya kuchagua wakandarasi wa miradi hiyo kutoa kazi kwa watu wasiokuwa na sifa na uwezo kifedha za kukamilisha shughuli wanazopewa.
“Sasa jamani tukiweka watu wabovu hapo ndiyo inakuwa shida kubwa ya kukamilika kwa miradi yetu ya maji lakini sasa na kuhusu maji tumesema tuweke wakala wa maji kama wa barabara ili asimamie kama Yule wa barabara”alifafanua mwakilishi huyo wa wananchi.
Mbunge Nagu hata hivyo alibainisha kuwa mpaka sasa bado serikali haijaweka wakala wa maji,kazi ambayo itafanywa katika kikao cha Bunge lijalo ili uwepo uhakika wa upatikanaji wa huduma hiyo ya maji safi na salama.
 Wanachama wa CCM wa Kijiji cha Diyagwa wakimpokea Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,Dk.Mary Nagu pamoja na msafara wake huku wakipeperusha bendera ya CCM kuashiria kutoridhishwa na kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama katika Kijiji hicho.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hanang,Methew Darema( wa pili kutoka kulia) akiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Hanang,Teddy Athumani(wa kwanza kutoka kushoto) na katibu wa UVCCM Wilaya ya Hanang,Ole Ngotick walipowasili katika Kijiji cha Dang'aida.
 Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu(wa kwanza kutoka kushoto) akionekana kufurahishwa na wimbo alioimbiwa na wananchi wa Kijiji cha Dang'aida kuhusu kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama huku wakimwonyesha maji machafu wanayokunywa.
Kikundi cha akina mama wakitumbuiza kwa wimbo uliokuwa ukipeleka ujumbe kwa Mbunge wa jimbo la Hanang pamoja na serikali ya wilaya hiyo kwa ujumla kuhusu  wananchi wanavyopata shida ya kufuata maji umbali mrefu huku yakiwa machafu. Habari na picha na Jumbe Ismailly.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...