THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Zoezi la Usajili Tigo Kili Half Marathon laendelea maeneo mbalimbali nchini

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kujisajili kushiriki mbio za Km 21 za Tigo Kili Half Marathon katika zoezi la usajili linaloendelea siku ya leo na kesho katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wateja wa Tigo wanaweza kujisajili kupitia namba *149*20# ili kushiriki mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi tarehe kupitia 8 Machi mwaka huu.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari kuhusu usajili wa Tigo kili half Marathon unaondelea siku ya leo na kesho katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wateja wa Tigo wanaweza kujisajili kupitia namba *149*20# ili kushiriki mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi tarehe kupitia 8 Machi mwaka huu.

Usajili na kuchukua namba za ushiriki wa Tigo Kili Half Marathon 2018 umeanza leo katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Watu wengi wa rika zote wamejitokeza leo kukamilisha usajili wao ili kukimbia mbio hizo za KM 5, Km 21 na KM 42 ambazo zitafanyika katika viwanja vya ushirika Moshi tarehe 8 Machi, 2018. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo ambapo usajili ulikuwa unaendelea, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa wateja wa Tigo wanaweza pia kujisajili kupitia namba *149*20#

 'Kujisajili, piga namba *149*20#   kisha fuata maelekezo rahisi ili ukamilishe usajili na kufanya malipo. Utapata ujumbe mfupi wa maneno (SMS) unaothibitisha muamala wako. Tunza ujumbe huo mfupi na kisha nenda nao pamoja na kitambulisho chako halisi katika vituo vilivyotajwa  ili kuchukua namba yako  ya ushiriki' alisema Woinde.

Vituo, tarehe na maeneo ambapo zoezi la kukamilisha usajili na kupokea namba ya ushiriki ni kama ifuatavyo; 
Dar es Salaam

TAREHE : 24 & 25 Februari - Jumamosi Na Jumapili.
MUDA: Saa Sita mchana hadi saa Kumi na Moja jioni
MAHALI: Mlimani City Mall karibu na Mgahawa wa Grano
 Arusha:

TAREHE: 27 & 28 February – Jumanne na Jumatano
MUDA: Kuanzia saa Nane Mchana hadi saa Mbili usiku.
MAHALI: Kibo Palace Hotel (Mlango wa Nyuma Parking )

Moshi

Tarehe: 01 March -  Alhamisi Saa Sita Mchana hadi saa Moja UsikuTarehe 02 March – Ijumaa Saa Nne Asubuhi Hadi saa Moja Usiku
Tarehe 3 March– Jumamosi Saa Tatu asubuhi hadi saa Sita Mchana
Mahali: Keys Hotel. Uru Road