Na Agness Francis Globu ya jamii
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC wanawakaribisha France Rangers katika dimba lao la nyumbani kwa ajili ya mchezo wa kirafiki.

France Rangers ni timu ambayo imemaliza msimu huu daraja la kwanza Mkoa wa Dar es Salaam yenye kikosi kizuri na wachezaji walio fiti uwanjani.

Mchezo huo wa kirafiki dhidi ya timu hizo mbili utachezwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi  utakaofanyika kesho Jumamosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Habari Azam FC Jaffary amesema pamoja na kikosi chao kinaendelea na mazoezi  kukabiliana na Mtibwa sugar katika mchezo wa robo Fainali kombe la  FA  machi 31 mwaka huu, mwalimu na benchi la ufundi kuweza kuwapima wachezaji kwa kuomba mechi ya kirafiki dhidi ya France Rangers ya Dar es Salaam.

"Ni sehemu tu ya benchi  la ufundi na mwalimu kuweza kuangalia baada ya mazoezi ya wiki moja na nusu pengine tu ni kutaka kuona kiwango cha  wachezaji pamoja na uwezo  wa kila mchezaji walichokielewa katika hazoezi hayo" amesema Jaffary.

Amesema katika mchezo huo watawakosa wachezaji wao mahiri wanne ambao ni Himidi Mau, Yahaya Zayd na Shabani Chilunda ambao wameitwa katika timu ya Taifa (Taifa Satars),mwengine ni Daniel Amor kutoka Ghana ambaye ni majeruhi.

"Mchezaji wetu nyota wa kimataifa kutoka nchini Ghana Daniel Amor anasumbuliwa na tatizo la goti, uongozi utamsafirisha  Amor  Siku ya  Jumatatu kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu" amesema Jaffary.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...