THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Hiki ndio kikosi cha Yanga kuelekea Botswana

KIKOSI Cha Mabingwa wa soka nchini na ambao wapo  kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara, Yanga SC , kimeondoka leo saa 10:15 alfajiri  kikielekea Nchini Botswana  kuwafuata Township Rollers ukiwa ni mchezo wa marudiano wa  michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Wachezaji 20 na viongozi 11 pamoja na wengine 8 ambao ni benchi la ufundi ambao wapo katika kikosi kamili cha msafara huo.


Ambapo katika mchezo uliopita uliokuwa wa aina yake kati ya timu hizo mbili ambao mtanange huo uliomalizika kwa dakika 90  na  Yanga alichezeshwa Makhirikhiri na kulazwa chali kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 

Katika Mchezo huo wa marudiano  wakilishi kutoka Tanzania Yanga anakabiliwa na kibarua kizito kwa kutakiwa kupata ushindi mnene ili kusonga mbele  na michuano hiyo. 

Mtanange huo wa  marudiano wa vuta nikuvute kati ya Mabingwa wa Tanzania bara Yanga dhidiTownship Rollers  utarindima huko Nchini Botswana tarehe 17 machi mwaka huu ikiwa kila timu ikihitaji  ushindi mnono ili kusonga mbele zaidi.