Akizungumza katika maadhimisho ya ‘Siku ya Wanawake Duniani’ yaliyofanyika leo Machi 8, 2018 katika kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, amesema wanawake ni nguzo muhimu ya kuinua familia  na wana mchango mkubwa katika kutekeleza majukumu ili kuziimarisha familia zao.
Mama Shein amesema akinamama wana mchango mkubwa katika kuimarisha familia ili zipate ustawi na kuzifanya zipige hatua zaidi ya maendeleo nchini, na kwamba wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa kila kunapotokea matatizo nchini yenye mwelekeo wa kupoteza amani.
Kwa hivyo amesisitiza haja ya kuendeleza ushirikiano katika kuendeleza amani na mshikamano ili kuhakikisha wanawake na watoto wanakuwa salama na kuishi bila khofu. Aidha, Mama Shein aliwataka akinamama na akinababa kushirikiana katika malezi bora ya watoto kulingana na maadili, silka na utamaduni wa nchi ili wawe raia wema.
Kuhusu vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinavyoendelea kushamiri kwa kasi, Mama Mwanamwema alisema Zanzibar bila ya uovu huo unaoathiri maendeleo ya taifa inawezekana iwapo jamii itakuwa kitu kimoja kwa kushirikiana kuvikomesha
Sambamba na hayo, alisema katika kupinga mapambano dhidi ya maradhi ya ukimwi, wanawake wana mchango mkubwa wa kudhibiti maambukizo ya virusi ifikapo mwaka 2030.
Lakini alieleza kusikitishwa kwake na kiwango kikubwa cha wanawake wanaoambukizwa maradhi hayo ambako kiko juu kuliko kwa wanaume.
“Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini ni mara mbili ya wanaume, hivyo tuchukuwe hatua madhubuti za kujiepusha na vitendo vinavyochangia kupata maradhi hayo,” alisisitiza.
Aidha aliwataka wanawake kuzitumia fursa za kujiunga na vikundi vya ushirika ili kujiimarisha kiuchumi kwa kujiongezea kipato na kupambana na umasikini, hali itakayoipa nguvu Serikali na washirika wengine kutanua wigo wa misaada yao.
 WAZIRI wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe. Maudline Cyrus Castico, akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliofanyika katika viwanja vya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani,huadhimishwa kila mwaka ifikapo March 8, maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.( Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...