ZUCKERBERG AFUNGUKA SAKATA  LA FACEBOOK.

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MWANZILISHI  na mmiliki wa mtandao wa Facebook  Mark Zuckerberg ameibuka na kuomba msamaha kwa wateja wake baada ya sakata la kudukuliwa kwa data za watumiaji  zaidi ya milioni 50 wa mtandao huo na kampuni ya taarifa na takwimu ya Cambridge Analytica. 

Kashfa hiyo imeipa hasara ya zaidi ya bilioni 45 kwa siku mbili kutokana na hofu na upotoshaji uliotokea kwa watumiaji wake. Zuckerberg amehaidi uaminifu na umakini zaidi wa kulinda data za watumiaji wake na hazitoingiliwa tena.

Sakata hilo linakuja baada ya utumikaji wa data wa watumiaji wa mtandao wa Facebook kudukuliwa na kutumika vibaya katika uchaguzi wa nchi za Kenya na Marekani (2016) ambapo Donald Trump aliibuka kidedea.

Mamlaka ya Cambridge analytica imemsimamisha kazi mkuu wake Cambridge Nix Alexander kwa kuhusika na sakata hili pia mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Cambridge  anayehusishwa na kampuni hii ya Uingereza ya utafiti data bado anaandamwa na kashfa ha kutengeneza Application iliyotumiwa kudukulia data na udukuzi huu ulimpa ushindi Donald Trump.

Imeelezwa kwamba Facebook ndio mtandao wenye watumiaji wengi zaidi duniani, ulianzishwa February 4 mwaka 2004 na Mark Zuckerberg na hadi kufikia mwaka 2010 ametangazwa kuwa miongoni mwa matajiri 100 duniani na mtu mwenye ushawishi zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...