Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SHIRIKA
la Umeme Tanzania (Tanesco)limekanusha taarifa inayosambaa kwenye
mitandao ya kijamii inayodai kutakuwa na tatizo katika mfumo wa
manunuzi ya LUKU kuanzia Machi 25 hadi Aprili 5 mwaka huu.
Taarifa hiyo ya kutunga inadai kutokana na hali hiyo wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho.
Tanesco
kupitia Ofisi ya Uhusiano imesema taarifa hizo si za kweli na uzushi
wenye nia ya kupotosha umma kwani haijatokea taarifa yoyote kuhusu
hitilafu katika mifumo ya manunuzi ya LUKU.
"Ikumbukwe
kwamba taarifa kutoka Tanesco hazitolewi na mtu binafsi bali ofisi ya
uhusiano iliyo chini idara ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo ni msimamizi wa
utoaji taarifa za shirika hili,"imesema taarifa ya Tanesco.
Imewaomba
wateja wote wa Tanesco waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote
."Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...