Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
TAASISI ya Taasisi ya Taswira ya Vijana Tanzania (TAVITA) imelaani vikali uchochezi unaofanywa na baadhi ya wanasiasa kupitia mitandao ya kijamii dhidi ya Serikali ya Awamu ya tano.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa TAVITA Otieno Peter amesema Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi kama vile kuanzisha miradi mikubwa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma.

Pia imejikita katika kusimamia rasilimali za nchi, kuhimiza uwajibika na kukomesha vitendo vya rushwa.Hivyo inasikitisha kuona baadhi ya watu wakitumia muda wao mwingi kuchochea uvunjifu wa amani badala ya kuelimisha jamii na endapo amani itapotea itakua imeharibu dira ya nchi yetu.

Ameviomba vyombo vya habari kutumia kalamu zao katika kuelimisha kuhusu masuala ya maendeleo kwa maslahi ya Taifa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa taasisi hiyo Shabani  Mwanga amewataka wananchi kutokubali taarifa zinazotolewa kwa ajili ya kuharibu taswira njema ya nchi kwani hao wanaofanya hivyo wanataka kuvuruga amani ya nchi iliyopo.

"Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mawakala ambao wanatumia saa 24 kutoa taarifa za kupaka matope ili kuharibu taswira njema ya taifa letu,"amesema .

Ameongeza taasisi ya Taswira ya Vijana Tanzania ipo tayari kupambana kwa hali yoyote na watu hawa wanaotaka kuchafua amani ya nchi na kwamba wapo tayari kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kwa maendeleo ya taifa.
 Katibu wa (TAVITA),Otieno Peter (kushoto) akizungumza kuhusu mambo ya maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano ikiwemo miradi ya kufufua umeme na ujenzi wa reli ya kisasa  leo jijini Dar es  Salaam. Kulia ni  Mwenyekiti wa TAVITA, Shabani Mwanga(kulia)
Waandishi wa habari wakimsikiliza  Katibu wa (TAVITA), Otieno Peter

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...