Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameupa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wiki mbili kwenda Pemba kukagua hali ya mawasiliano ya simu za mkononi na kuwasilisha taarifa hiyo ofisini kwake.
Mhandisi Nditiye ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Zanzibar ya kukagua hali ya mawasiliano kisiwani humo na kutembelea taasisi za mawasiliano zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo suala la mawasiliano ni la muungano.
Nditiye amesema kuwa amepokea taarifa kutoka kwa wabunge wa Kisiwa cha Zanzibar kuwa hali ya mawasiliano kwenye kisiwa hicho sio nzuri na sehemu nyingine hakuna mawasiliano licha ya kuwa kuna minara ambayo inatoa huduma za mawasiliano ila kutokana na jiografia ya Pemba ambapo kuna milima na mabonde hivyo mawasiliano si ya uhakika. “Nawaagiza muende Pemba mkaainishe maeneo yote ambayo hayana mawasiliano na muwasilishe taarifa hiyo ofisini kwangu baada ya wiki mbili,” amesema Mhandisi Nditiye.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar Bi. Esuvatie-Aisa Masinga wakati akiwasilisha taarifa yake kwa Mhandisi Nditiye kuhusu majukumu ya ofisi yake ya usimamimizi na udhibiti wa mawasiliano na posta, amekiri kuwa yapo baadhi ya maeneo Pemba na Unguja ambapo hali ya mawasiliano sio nzuri na hairidhishi.
 Meneja Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Zanzibar, Bi. Esuvatie-Aisa Masinga akitoa taarifa ya hali ya mawasiliano Zanzibar kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara yake kisiwani humo
 Meneja Msaidizi Mtandao wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Zanzibar Bwana Mohamedi Ali Haji akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) njia yanakopita mawasiliano kutoka Dares Salaam kuja Zanzibar wakati wa ziara yake kisiwani humo
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ( wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini maelezo kutok akwa mfanyakazi wa TTCL kuhusu mwitikio wa wateja kwa huduma zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakati wa ziara yake Zanzibar
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akitoa maelekezo kwa mwakilishi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bwana John Munkondya kuhusu vituo vya mawasiliano vilivyopo Zanzibar wakati wa ziara yake kisiwani humo.
 Mfanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Zanzibar, Bwana Khalfan Mmkahirika akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano namna scanner inavyofanya kazi ya kukagua mizigo na vifurushi vinavyosafirishwa na Shirika hilo ndani na nje ya nchi ili kulinda usalama wa raia na taifa wakati wa ziara yake Zanzibar. Mwenye koti nyeusi ni Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika hilo Bwana Hassan Mwang’ombe.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara yake kwa taasisi za mawasiliano Zanzibar. Kushoto ni Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika hilo Bwana Hassan Mwang’ombe na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) Bwana Hussein Selemani Nguvu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...