WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa za Afrika kutoa mapendekezo ya namna ya kutokomeza magonjwa yasiyo ambukiza kwa wakuu wa nchi hizo ili yafanyiwe kazi.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Machi 19, 2018) wakati akifungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC)

Alisema magonjwa yasiyo ambukiza ni miongoni mwa magonjwa ambayo yameendelea kuwatesa wananchi kwa kiasi kikubwa katika nchi nyingi za Bara la Afrika, hivyo vema mawaziri hao wakatoa mapendekezo ya namna ya kuyatokomeza.Waziri Mkuu alisema magonjwa hayo yanaweza kudhibitiwa kwa kuhamasisha wananchi kuboresha lishe na kusisitiza ulaji wa vyakula bora, kufanya mazoezi na kubadili mitindo ya maisha.

“Magonjwa yasiyoambukiza yanaongoza kwa kusababisha vifo katika baadhi ya nchi wanachama wa ECSA. Magonjwa haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya mfumo wetu wa lishe na maisha, hivyo ni muhimu suala hili likatafutiwa ufumbuzi.”

Waziri Mkuu alisema magonjwa yasiyoambukiza pamoja na magonjwa mengine ya milipuko kama ebola, homa ya bonde la ufa, dengue, homa ya manjano yamekuwa kikwazo cha maendeleo kwa katika baadhi ya nchi.

Pia, Waziri Mkuu aliongeza kuwa sekta ya afya ni muhimu kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya nchi zote zikiwemo zilizoendelea na zinazoendelea, hivyo changamoto zote zinazoikabili zinapaswa zipewe kipaumbele katika utatuzi.Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu alisema malengo ya mkutano huo ni kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazohusu sekta ya Afya na kuyapatia ufumbuzi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri wa Afya kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ambazo ni Tanzania, Malawi, Lethoto, Uganda, Kenya, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Muwakilishi kutoka nchini Mauritious.Pia Katibu wa jumuiya hiyo Profesa Yoswa Dambisya, Muwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Paolo Belli pamoja na wadau wa sekta ya afya kutoka nchi hizo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MACHI 20, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Afya wa Uganda .Sarah Opendi ,wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) kushoto ni Wazri wa Afya wa Malawi Atupele Muluzi,Waziri Mkuu amefungua mkutano huo jana March 19, 2018 Jijini Dar es salaam.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) 
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...