Na Ripota Wetu, China
BALOZI wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema zaidi watu 1,000 wamepata fursa ya kutembelea banda la Tanzania ambalo lilikuwepo kwenye maonesho ya utalii nchini humo.

Idadi hiyo ya watu ambao wametembelea banda la Tanzania imesaidia kuwapatia taarifa sahihi na za kutosha kuhusu utalii wetu na ni moja ya eneo ambalo limetumika vema kutangaza vivuto vilivyopo.

Balozi Kairuki ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye maoesho ya utalii yaliyofanyika nchini China ambayo yamemalizika hivi karibuni.

Akifafanua zaidi kuhusu Maonyesho ya biashara ya Utalii (China Outboard Travel & Tourism Market COTTM) yaliyomalizika hivi karibuni jijini Beijing China Balozi Kairuki amesema maonesho hayo yamekuwa na mwitikio mkubwa.

"Zaidi ya watu 1,000 wameweza kutembelea banda la Tanzania hatua ambayo imesadia watu wengi kupata taarifa za kutosha kuhusu fursa za Tanzania.Naipongeza bodi ya utalii na mamlaka zote za utalii Tanzania pamoja na mawakala wa utalii ambao walishiriki kwa lengo la kuchangamkia fursa hiyo,"amesema.

Ameogeza soko la China ni jipya na linalokua kwa kasi,hivyo matarajio yao hizo taasisi za bodi ya utalii, Hifadhi ya Ngorongoro ,TANAPA watapewa nguvu zaidi, watawezeshwa kibajeti ili wakushiriki maonyesho mengi zaidi hapa China.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki (Kushoto) akishiriki mahojiano maalumu yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga cha   "Chinese Satelite Travel" chenye  watazamaji zaidi ya Milioni 100 ndani na nje ya China. Mahojiano hayo yaliongozwa na Bi. Mei Qing  mtangazaji maarufu wa Television hiyo.
 Afisa Utalii kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, Piter Makutian (Kushoto) akizungumza jambo katika  mahojiano maalumu yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga  cha   "Chinese Satelite Travel" chenye  watazamaji zaidi ya Milioni 100 ndani na nje ya China. Mahojiano hayo yalifanyika wakati wa Maonyesho ya Utalii yaliyofanyika Beijing China mapema wiki hii. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki.
 Mahojiano yakiendelea  yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga  cha   "Chinese Satelite Travel"
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mahojiano kwenye kituo cha runinga  cha  "Chinese Satelite Travel" 
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(kushoto) akipata maelezo kuhusu Maonyesho ya Utalii  kutoka kwa Afisa Utalii Mwandamizi - Hifadhi ya Taifa Tarangire Theodora Aloyce (katikati), Wa pili kushoto ni Afisa Utalii habari  - Bodi ya Utalii Tanzania, Irene  Mville, Afisa Utalii- Mamlaka ya Hifadhi  ya Eneo la Ngorongoro, Piter Makutian (wa pili kulia) na Afisa Kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China, Lusekelo Gwassa
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi Watanzania nchini China, Remidius Emmanuel(Kushoto)  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Compass Safari, Peter Larocque inayofanya kazi zake nchini Tanzania.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...