Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Ndg. Andrew W. Msssawe amekutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga na kusisitiza umuhimu wa kukamilisha Usajili wananchi mkoani humo mwezi Mei mwaka huu ili NIDA kupata muda wa kutosha kufanya uhakiki na mapingamizi kwa wale wote waliosajiliwa; na kuwezesha Mamlaka kuzalisha vitambulisho kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga kukagua maendeleo ya zoezi la Usajii na Utambuzi wa Watu linaloendelea; akiwa ameambatana na Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Ndg. Alphonce Malibiche, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi.Rose Mdami na Ndg. Steven Kapesa Mkuu wa Kitengo cha Vihatarishi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo; Katibu Tawala wa Mkoa huo Ndg. Albert Msovela amesema mkoa wa Shinyanga una changamoto kubwa ya wahamiaji haramu hususani Wilaya ya Kahama na kwamba wamejipanga Usajili katika eneo hilo kufanyika kwa uangalifu mkubwa kwa kuhusisha vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.
Viongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kikao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwasajili wananchi na kumaliza zoezi kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. ,Andrew W. Massawe akiweka saini kwenye kitabu cha wageni, mara alipowasili kwenye ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga. Pembeni ni Katibu Tawala huo Ndg Albert Msovela
Wananchi wa Kijiji cha Usanda Kata ya Tinde mkoani Shinyanga walivyokutwa kwenye foleni ya Usajili Vitambulisho vya Taifa kwenye zoezi linaloendelea mkoani humo wakati wa ziara ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu aliyoifanya hivi karibuni.
Bi. Magdalena E. Ngosha mkazi wa kijiji cha Usanda Kata ya Tinde akichukuliwa alama za vidole na Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea kijijini hapo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...