Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amelitaka Baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwa na mbinu mbadala ili kuiwezesha mamlaka hiyo kujiendesha  pasipo kutegemea bajeti kutoka Serikali Kuu.

Pia amelitaka baraza hilo kujithamini kwanini viwanja vilivyopo hapa nchini havipo miongoni mwa viwanja 10 bora  Afrika na kuwataka  waandae  mkakati wa kuiwezesha viwanja hivyo kuingia katika ushindani wa kimataifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya  kuzindua  baraza la sita la wafanyakazi wa TAA, Prof.Mbarawa, aliyekuwa mgeni rasmi amesema haiwezekani viwanja vya ndege vilivyopo hapa nchini vikose uwezo binafsi wa kujiendesha wakati kuna fursa nyingi za kuipatia mamlaka hiyo mapato.

“Lazima mjiulize kwanini hadi leo kununua gari ndani ya uwanja wa ndege mnasubiri fedha kutoka Serikali kuu wakati katika viwanja hivi kuna sehemu mmepangisha watu fedha zinaenda wapi"

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA Richard Mayongela amesema  mpaka sasa wamenunua magari sita kutoka kwenye mfuko wa TAA ili kuongeza ufanisi katika kazi za kila siku.

Amesema wamefanikiwa kupata fedha ya kujenga ukuta kwenye kiwanja cha ndege cha Mwanza ili kuzuia wananchi kupita kwenye uwanja huo.

"Leo tunazindua baraza la sita la wafanyakazi wa TAA ili kuongeza ufanisi kwenye viwanja vyetu vyote hapa nchini na asiyefanya kazi kwa ufanisi atawajibika,"amesema Mayongela.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza jambo alipokuwa anafungua mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela akizungumza mafaniko waliyoyapata pamoja na kuelezea changamoto wanazozipata wakati wa mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa baraza anayemaliza muda wake na pia ni Kaimu  Meneja rasilimali watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) akizungumza jambo wakati wa mkutano wa sita wa mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa  alipokuwa anafungua mkutano  wa baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mara baada kuzindua mkutano huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...