MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam Maulid Mtulia
(CCM), ametembelea maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko ya
maji huku akitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi wa jimbo
hilo ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine na mvua
za masika huku akiishauri Halmashauri Manispaa ya Kinondoni
kutafuta suluhu ya kudumu ili wananchi wabaki salama.
Pia amesema mbali ya kutoa pole atatumia fedha za Mfuko wa
Jimbo kwa ajili ya kukodisha mashine za kunyonya maji pamoja na
fedha ya kununua mafuta ili maji ambayo bado yapo kwenye
makazi ya wananchi wake yaondolewe huku akitoa katazo la watu
wasiendelee kujenga kwenye bwawa la Tengeza wala kutupa taka
kwani athari zake ni kubwa kwa wananchi walio wengi.
Mbunge Mtulia amesema hayo jana jimboni kwake Kinondoni
baada ya kufanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa
na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la
Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa ambapo pia ameshuhudia
baadhi ya watu kujenga makazi kwenye bwawa la Tengeneza na
matokeo yake maji kukosa pakwenda na hivyo kuharibu makazi ya
watu.
Pia ametembelea baadhi ya nyumba za wananchi wa maeneo hayo
ambapo zaidi ya asilimia 70 ya makazi ya watu yamekumbwa na
mafuriko ambapo akatumia nafasi hiyo kuiomba Halmashauri ya
Kinondoni kurekebisha mitaro iliyopo ili maji yapite kwa urahisi
huku akitoa ombi la kuchimbwa kwa mitaro mikubwa ambayo
itakuwa suluhu ya maji kutokwenda kwenye makazi ya watu kama
ilivyo sasa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa , mtaa wa Msisiri A Jumanne Mbena akielezea changamoto za mafuriko ambazo zimesababishwa na baadhi ya wananchi kujenga kwenye Bwawa Tengeneza lililopo eneo la Msisiri A kwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akifanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo am bayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
Muonekano wa maji yaliyozingira nyumba za wakazi wa Kata za Msisiri A na B na Kambangwa katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akipita kwa tabu wakati alipofanya ziara ya kukagua mae neo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akiangalia moja ya madimbwi yaliyojaa maji mtaani alipo fanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...