Na Anthony Ishengoma WAMJW
Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGOs Marcel Katemba amewataka Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzisimamia NGOs ili zifanye kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha Wasajili Wasaidizi ili kutoka mafunzo kwa ajili ya kukumbashana majukumu yao Kama wasajili wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Amesema kuwa kimsingi Mashirika yasiyo ya Kiserikali bado hayatambui umuhimu wenu hivyo tutawakutanisha na Mashirika haya kwa ajili kufahamiana kiutendaji na kutambuana.
Aidha Katemba amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakati mwingine yanakosa majibu muhimu kutoka kwa Wasajili Wasaidizi hivyo kusababisha waone kuwa Maafisa Maendeleo ya Jamii sio watu sahihi kusimamia shughuli zao.
"Lengo la Mafunzo haya nikukumbashana mambo muhimu ambayo yatawafanya muweze kutoa majibu stahiki kwa Mashirika haya na kuyasimamia ipasavyo baada ya kujua shughuli wanazozifanya"alisisitiza Bw. Katemba.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika hayo
Bw. Marcel Katemba akizungumza na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo
ya Kiserikali kutoka katika Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Dar es
Salaam katika kikao baina yake na Wasajili Wasaidizi hao na wadau wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilicholenga kuboresha namna bora ya
uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
Baadhi
ya Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Dar es
Salaam wakifuatilia mada na mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yakitolea na
Msajili wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha kujadili namna
bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo kilichofanyika katika
Ukumbi wa Karimjee.
Mkurugenzi
Msaidizi Usajili wa NGOs Bw. Baraka Leonard na Mkurugenzi Msaidizi
Ufuatiliaji Bi. Tausi Malima wakijadiliana jambo wakati wa kikao kazi
kati ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Wasajili wasaidizi
wa Mashirika hayo mkoani Dar es Salaam kilichofanyika katika Ukumbi wa
Karimjee kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika
hayo mkoani humo.
Mkurugenzi
wa Msaidizi Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornald Baraka
akiwakumbusha washiriki mambo muhimu yanayohitaji kuzingatiwa kabla na
baada ya kusajili Shirika Lisilo la Kiserikali kwa Wasajili wasaidizi wa
Mashirika hayo kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam
katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali, Wasajili Wasaidizi kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee
kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani
humo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...