THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

RAIA WA KIGENI WATAKIWA KUACHA KUINGILIA ZOEZI LA UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA

Editha Karlo,Kasulu.

MWENGE wa Uhuru 2018 unaondelea na mbio zake katika Mkoa wa Kigoma umewataka raia wa kigeni kuacha kuingiliza zoezi la uandikishwaji wa vitambulisho vya Taifa  linaloendelea sasa Mkoani humo, kwakuwa zoezi hilo ni haki ya Watanzania.

Mmoja wa wakimbiza mwenge Kitaifa   Dominik Njunwa  aliyasema hayo wakati akitoa ujumbe wa Mwenge, Katika Kijiji cha Shunga  Wilayani Kasulu wakati wa ufunguzi wa bwalo la kulia chakula katika Shule ya Sekondari Muyovozi, ambapo aliwaomba Watanzania waishio jirani na Nchi ya Burundi kuwafichua wale wote wasio Raia wa Tanzania  watakao jitokeza kujiandikisha katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa.

Njunwa alisema hairuhusiwi Raia yeyote asie Mtanzania kujiandikisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vya Taifa, kwakuwa vitambulisho hivyo vinatolewa kwa Watanzania pekee na ni kosa kubwa kwa Raia wa Nchi nyingine kupata kitambulisho hicho .

 Kaimu Mkuu  wa Wilaya  ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala aliwataka viongozi wa Vijiji na mitaa kuacha kuhujumu zoezi hilo la kuandukisha vitambulisho vya Taifa  kwa kuwaingiza watu wasio Watanzania iliwaweze kupata vitambulisho kwa atakae bainika anafanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa Wilaya  aliwataka wananchi kuwafichua wale wote wanaowahofia kuwa sio Raia wanaojitokeza kujiandikisha kwa ajili ya Kupata vitambulisho vya Taifa na kuwaripoti kwa vyombo husika ili kuweza kuchukuliwa hatua za Kisheria na waondolewe katika zoezi hilo.

Kanali Ndagala alisema zoezi hilo ni kwa Watanzania tu wanapopatiwa vitambulisho,Raia wasio wa Tanzania ni kosa na inaweza kuleta shida katika Taifa la Tanzania na Kuwaonya kuwa makini ili kuendeleza hali ya usalama hasa Kwa Mikoa iliyopo karibu na Nchi jirani za Burundi na Congo.

" Kuanzia Mwakani  Mtanzania akiwa na kitambulisho cha Taifa  anauwezo wa Kupata hati ya kusafiria wanapopata watu wasio Raia wakipata hati zetu za kusafiria inatupa shida sana na wanatumia kwa kufanya uhalifu jambo ambalo sio zuri katika Taifa letu marufuku kabisa kwa raia asie Mtanzania kuchukua Kitambulisho cha utaifa ", alisema Ndagala.

Mwenge wa Uhuru Wilayani Kasulu umekagua na Kuzindua Miradi 13 yenye thamani ya zaidi ya bilioni tano  miradi hiyo ni ya Maji, Afya na Maji na sambamba na Miradi hiyo Mwenge huo umezindua Kituo cha Afya Katika Kijiji cha Shunga kilicho jengwa na Kanisa la Agrikana  Dayosisi ya Westeni Tanganyika.
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2018 Charles Kabeho akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa Wakazi wa kijiji cha Nyamidaho Wilayani Kasulu baada ya mwenge kuzindua mradi huo wa maji
Kiongozi wa mbio za mwenge 2018 Charles Kabeho akifungua Club ya wapinga rushwa katika sekondari ya Titye Wilayani Kasulu