THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa mafuriko na kuwataka wananchi waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuokoa maisha yao. RC Makonda amesema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 7 wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo ambapo amesema njia pekee iliyobaki ni wananchi kuchukuwa tahadhari.
Kufuatia mwendelezo wa mvua hizo RC Makonda ameziomba mamlaka husika kusimamisha masomo kwa muda wa siku mbili ili kuwaepusha wanafunzi kukumbwa na Maafa. Aidha RC Makonda amesema serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya na mvua ikiwemo madaraja, Barabara,shule pamoja na kuzibua mitaro.
Akiwa Mtaa wa Mfaume Kata ya upanga RC Makonda ameshuhudia jengo la gorofa kumi likiwa limepata hitilafu ya kutitia ambapo ameagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina na kuwasihi wakazi wa jengo hilo pamoja na majirani kutafuta sehemu ya kujisitiri kwa wakati huu kwa mustakabali wa usalama wao. 
Pamoja na hayo RC Makonda amewahimiza wananchi kufuatilia tahadhari zinazotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa nchini pamoja na vyombo vya habari.