Na Tiganya Vincent
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack amewataka wakazi wa Mkoa wa Tabora kutunza na kulinda mistu ya asili na miti inayopandwa sasa hivi ili ikuyafanya mazingira kuwa endelevu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema kama watafanya mchezo na kuacha baadhi yao watu waingie ndani ya mistu na kukatakata ovyo rasilimali za mistu upo uwezekano wa hali kuwa mbaya  na kukosa hata mvua kidogo zinapatikana hivi sasa kutokana na kutoweka kwa mistu.

Telack alitoa rai hiyo jana mjini Tabora wakati akifunga kongamano la siku la mazingira ambalo liliwahusisha wadau mbalimbali likiwa na lengo la kuweka maazimio ambayo yatasaidia katika kupambana na uharibifu na mistu.

Alisema kama wanataka kuona athari za uharibifu wa mazingira , wanatakiwa kwenda kuangali Shinyanga ilivyoathirika na ukataji ovyo wa miti katika Wilaya mbalimbali kama vile Kishapu.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa ni vema wananchi wakaungana na viongozi na wadau wengine kuwakemea wale wote wanaingia katika mistu na kukata miti hivyo hata bila ya kuwa na vibali vya viongozi.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku wa mazingira uliofanyika jana mjini Tabora. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akifungua jana kongamano la siku moja la wadau mbalimbali la kujadili masuala ya kuboresha hali ya ulinzi na usalama mkoani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack  akisisitiza jambo wakati wa kufunga mkutano wa siku wa mazingira uliofanyika juzi(jana) mjini Tabora.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi na kushoto ni Mkiuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri. Picha na Tiganya Vincent.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...