NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewaomba viongozi wa dini mbalimbali kusaidia kuwaelimisha waumini wao juu ya umuhimu wa watoto wenye umri wa miaka 14 kupatiwa chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi ili wajitokeza kwa wingi kupatiwa huduma hiyo kuanzia wiki ijayo.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati anafungua semina ya siku moja ya Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi ya Mkoa huo.Alisema viongozi hao wanayo nguvu kubwa na wafuasi wengi wakitumia fursa hiyo watasaidia kufikisha ujumbe sahihi na kwa wakati na hivyo kuokoa maisha ya wanawake hapa baadaye.

Mwanri alisema ugunduzi wa Chanjo hiyo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine) ni habari njema ambayo inapaswa kuwafikia wananchi wengi ili waweze kuwapeleka watoto wao wa kike kwa ajili ya kuwakinga na ugonjwa wa saratani ya mlango ambao umekuwa ukisababisha upotevu wa maisha ya wanawake wengi.



Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua jana semina ya siku moja ya Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi ya Mkoa huo ikiwa ni maandalizi ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi itakayoanza tarehe 23 Mwezi huu mkoani kote.

Viongozi wa dini mbalimbali na wageni waalikwa wakiwa katika semina ya siku moja ya Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi ya Mkoa huo ikiwa ni maandalizi ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi itakayoanza tarehe 23 Mwezi huu mkoani kote.Picha na Tiganya Vincent.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...