Assalaam Aleikum.
Salaam zangu za Mei Mosi
Kwanza sote tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma anaendelea kutupa uhai na uzima hadi siku ya leo.
Hakika pumzi hii ndio inatufanya
tufurahi na kuhuzunika pamoja,pia ndio inayotufanya tuweze kuandika na
kusoma maandiko mbalimbali ikiwemo andishi hili dogo
Jana pale uwanja wa taifa palifanyika
mechi kubwa kabisa ktk ukanda huu wa Afrika Mashariki. Simba na Yanga
zote za hapa jijini Dar.
Sio vyema kurejea kuwapa matokeo ila
Alhamdulillah klabu yangu ya Simba imefanikiwa kushinda na kujisogeza
karibu kabisa na ubingwa wa ligi kuu nchini
Nimeandika kujisogeza kwa kuwa bado
hatujatwaa ubingwa.kwa sasa tunahitaji points tano tu ili tuweze
kutawazwa ubingwa huu unaosubiriwa kwa hama na washabiki wote kote
nchini
Kiukweli hzi points tunazohitaji
tutazisaka kwa tahadhari zote na kwa kutambua kiu ya wanasimba..
tutaingia kwenye michezo ilobaki kwa nguvu kubwa na kwa umakini wa hali
ya juu,sambamba na kuwaheshimu wapinzani wetu
Ukiachana na hayo nna vitu vwili very special nataka kuvisema hapa
Kwanza ni shukran kwa washabiki wetu..ktk maisha yangu yote nilioishi sijapata kuona washabiki kama wa Simba..
Ni watu wasikivu mno na wenye subira na
upendo wa hali ya juu,ni watu wanaopenda futboll halaf ndio timu
yao,wana ustaarabu uliopitiliza na wenye mapenzi yasio na shaka kwa
klabu yao,
Kwenye ustaarabu huwa natolea mfano wa
kitendo cha kutoa back pass kwa mchezaji Hassan kesi wakati akiichezea
Simba kwa Donald Ngoma wa Yanga na kutufunga goli la kizembe zaid ktk
historia ya derby hii
Inawezeka kabisa ilikuwa ni bahati
mbaya,ila kilichostaajibisha muda mchache ujao mchezaji huyo alihamia
Yanga tena kwa maneno mabaya ya dharau na kebehi..naapa Wallah kitendo
kile ingekuwa kwa wenzetu kessi angeuhama mji huu na kurudi Morogoro
(tamka Mrogoro)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...