Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Ujenzi ya Nchini China ya Civil Engineering Construction Corporation 'CCECC' Bw. Zhuang  Shangbiao alisema hatua iliyochukua  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  'SMZ' ya kuipa kazi ya ujenzi wa barabara Nchini imeleta heshima kubwa na ya kipekee kwa Kampuni hiyo.

Alisema kazi iliyo mbele kwa uongozi na wahandisi wa kampuni hiyo hivi sasa ni kujipanga vyema katika kuhakikisha heshima waliyopewa na SMZ wanailinda katika kuwajibika ipasavyo  wakati wa utekelezaji wa jukumu hilo zito katika misingi ya ari na bidii kubwa.

Bwana Zhuang  Shangbiao akiuongoza Ujumbe wa Viongozi saba wa Taasisi hiyo ya Civil Engineering Construction Corporation alisema hayo wakati akitoa shukrani katika mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema uzowefu wa ujenzi iliyokuwa nayo Kampuni hiyo ya CCECC kwa zaidi ya Miaka 50 iliyopita inahamishiwa Zanzibar  katika ujenzi wa barabara inayoanzia Bububu, Mahonda  kupitia  Kinyasini hadi Mkokotoni yenye urefu wa Kilomita 31.

Bwana Zhuang alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wahandisi wa Ujenzi wa Kampuni ya CCECC watakamilisha kazi hiyo kwa wakati ulliopangwa na katika kiwango kinachokubalika Kimataifa kwa vile wana utaalamu na uzoefu wa kutosha.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya Civil Engineering Construction Corporation 'CCECC' ya China Bw. Zuang Shangbiao Vuga Mjini Zanzibar.
 Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China Bw. Zuang Shangbiao wa tatu kutoka Kulia akielezea shukrani zake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwa kuiamini Kampuni yake kujenga Bara bara ya Bububu hadi Mkokotoni kupitia Mahonda na Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.  Mohamed Aboud Mohamed.
  Balozi Seif kushoto akisifu umahiri wa Kampuni za Kichina zinazofanya kazi Nchini Tanzania wakati akibadilishana mawazo na Rais wa Kampuni ya CCECC Bw. Zhuang Shangbiao aliyekaa upande wa Kushoto.
 Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China Bw. Zuang Shangbiao Kushoto akimkabidhi zawadi ya picha ya Ukuta Mkuu wa China 'Great Wall' Balozi Seif mara baada ya mazungumzo yao.
 Bwana Zuang Shangbiao Kushoto akifurahia zawadi ya  viungo aliyokabidhiwa na Balozi Seif baada ya mazungumzo yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...