Na Ripota Wetu, Blogu ya jamii
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo ameanza ziara rasmi nchini China yenye madhumuni ya kudumisha ushirikiano wa kijeshi kati ya Tanzania na China.

Taarifa kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa Jenerali Mabeyo ameanza ziara Mei mwaka huu na hiyo inatokana na mwaliko wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China.Akiwa huko atafanya mazungumzo rasmi na Mkuu wa Majeshi wa China Jenerali LI Zuocheng. Aidha, atakutana na Waziri wa Ulinzi wa China Jenerali WEI Fenghe kesho.

"Baada ya kuwasili nchini China Mei 20 Mei mwaka huu, Jenerali Venance Mabeyo alitembelea Ubalozi wa Tanzania nchini China ulioko mjini Beijing, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Maofisa wa Ubalozi wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika Mazungumzo hayo Balozi Kairuki amemueleza Jenerali Mabeyo, hali ilivyo nchini China kwa sasa katika nyanja mbalimbali zinazogusa uchumi, jamii za watu wa China na siasa, na nafasi ya nchi ya China kimataifa kwa sasa.

Aidha, Balozi Kairuki amefafanua hali ya maendeleo ya ushirikiano wa Tanzania na China kisekta na ujumla wake, pamoja na utekelezaji wake.

Kwa upande wake Jenerali Mabeyo, licha ya kueleza madhumuni ya ziara yake hiyo, pia alizungumzia hali ya sekta yake, na nafasi ya ushiriki wake kwenye utekelezaji wa majukumu ya Ulinzi na Usalama nchini.

Katika ziara hiyo, Jenerali Venance Mabeyo ameambatana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika kikao cha mazungumzo na  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa Kairuki, pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Ubalozi wa Tanzania nchini China.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo(kulia) akimkabidhi zawadi  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki(kushoto) alipotembelea ubalozi wa Tanzania nchini China.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki (Kulia).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja  na  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki, Maofisa waandamizi kutoka  Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Maofisa wa Ubalozi.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na  Maofisa waandamizi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini China, Maofisa wa Ubalozi pamoja na uwakilishi wa Watanzania wanaosoma nchini China.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...