Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetupilia mbali maombi ya upande wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe ya kutaka kesi yao ikasikilizwe Mahakama Kuu.

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Hakimu Mashauri amesema kuwa amepitia hoja zote za utetezi na upande wa mashtaka, ambapo ameona hoja za upande wa mashtaka hazina mashiko."Natupilia mbali hoja za upande wa mashtaka kwamba kesi iende Mahakama Kuu," amesema ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi May 16,2018 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa Maelezo ya awali, (PH).

Miongoni mwa hoja za utetezi kutaka kesi hiyo ipelekwe Mahakama Kuu ni kwa sababu kuna uvunjifu wa haki ya msingi ya Kikatiba. Pia shtaka la pili linalowakabili washtakiwa katika hati ya mashtaka linakiuka haki ya msingi ya washtakiwa ya kufanya shughuli za kisiasa za chama wanachotoka cha Chadema.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina Akwiline

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni, mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.Mbunge wa Tarime mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.
Kwa upande wa Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Ester Bulaya hawakuwepo mahakamani ambapo Wakili Peter Kibatala alieleza kuwa walikuwa safarini kutoka Bungeni Mjini Dodoma kuja Dar es Salaam kuhudhuria kesi lakini wakaharibikiwa na gari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...