NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA.

Mkazi wa Mtaa wa Nyerere A katika Kata ya Mabatini wilayani Nyamagana katika Jiji la Mwanza, Fred Kaseko (47) amepata msaada wa baiskeli ya miguu mitatu (wheel chair) itakayomsaidia kwa usafiri.

Kaseko alipata ulemavu wa miguu uliosababishwa na ajali ya gari miaka tisa iliyopita na kusababisha ashindwe kutembea baada ya miguu kukosa mawasiliano kutokana na neva za mgongo kuathiriwa.

Akipokea msaada huo jana uliotolewa na familia ya Mohamed Abass Mahamoud Abbas Mohamud Damji yenye asili ya Kiasia ya jijini Dar es Salaam,Kaseko alisema ameteseka kwa miaka tisa akitembea kwa kujivuta kwa kutumia mikono.

Alisema alipata ajali na taratibu miguu ilianza kupoteza uwezo wa kutembea wala kusimama na alipokwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) na kufanyiwa vipimo iligundulika kuwa disc za mgongo zilikuwa zimekandamiza mishipa ya fahamu baada ya kupata ajali.
 Fred Kaseko , mkazi wa Mtaa wa Nyerere A Mabatini kabla ya kupata msaada wa baiskeli ya miguu mitatu alikuwa akitambea kwa kutumia  mikono.
 Sheikh wa Bilal Muslimu Mission of Tanzania Hashim Ramadhan (kulia) akimkabidhi baiskeli ya miguu itatu Fred Kaseko.Nyuma ni familia ya Kaseko ambaye anasumbuliwa na miguu kupooza baada ya kupata ajali. Baiskeli hiyo imetolewa na familia ya Mohamed Abass Mahamoud Damji . Picha Na Baltazar Mashaka.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...