Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola ametoa muda wa miezi sita kwa kiwanda cha HUACHENG kinachojihusisha na uchinjaji na usafirishaji wa nyama ya Punda Mkoni Dodoma kuondoa mabaki ya miundo mbinu ya vyuma na mbao ambavyo awali vilikua vikitumika katika uchinjaji wa ngo'mbe.

Mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika kiwanda hicho iliyolenga kufuatilia maagizo ya Serikali yaliyotolewa hapo awali, Waziri Lugola ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kutafuta wawekezaji ambao wanaweza kutumia miundo mbinu hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi. "Mvua itakaponyesha mahali hapa patakuwa na uchafuzi wa hewa, na kwetu sisi wana mazingira magofu kama haya ni uchafuzi wa mazingira, hivyo ndani ya miezi sita kama hamjapata ufumbuzi, ondoweni mabaki haya". Lugola alisisitiza.

Aidha, Kiwanda hicho kimetakiwa kufuata takwa la kisheria la kufanya Ukaguzi wa Mazingira kwakuwa awali kiwanda hicho kimekua kikifanya shughuli zake bila kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira. Waziri Lugola ameupa uongozi wa Kiwanda hicho muda wa miezi miwili kukamilisha takwa hilo kama lilivyoainishwa katika Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.

Katika ukaguzi huo Waziri Lugola amegundua pia kiwanda hicho hakina Mpango Endelevu kama Sheria inavyoelekeza, hivyo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeagizwa kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo ndani ya miezi miwili.

Msemaji wa Kiwanda hicho Bw.Michael Gao amesema kuwa maagizo hayo yatatekelezwa kikamilifu na kwa muda uliotolewa. Kiwanda hicho huchinja punda ishiriki kila siku na wanasafirishwa kupelekwa katika Nchi za China na Vietnam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola mwishoni mwa wiki ameendelea na ziara ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira. Pichani akipata maelezo kutoka kwa Afisa Afya wa Jiji Bw. Carle Lyimo mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuchinja punda cha HUACHENG kinachomilikiwa na raia wa China.
Mganga wa Mifugo Bw. Merjoly Mariki Msimamizi wa viwanda vya nyama Kanda ya Kati akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Naibu Waziri Mhe. Kangi Lugola mara baada ya kukagua kiwanda cha kuchinja Punda eneo la Kizoto Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa taka.
Mabaki ya miundo mbinu ambayo awali ilikua ikitumika katika kuchinja ngombe katika kiwanda cha HUACHENG Jijini Dodma ikiwa imetelekezwa baada ya mwekezaji huyo kutoitumia tena na kujishughulisha na uchinjaji wa punda.
Sehemu ya punda wakisubiri kuchinjwa, imeelezwa kuwa nyama ya punda hao ina soko kubwa sana katika Nchi za China na Vietnam. Wastani wa punda ishiriki huchinjwa kila siku katika Kiwanda hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...