Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania(T FDA ) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali Afrika wamebuni miradi mikubwa miwiliyenye lengo la boresha,kuhakiki na kufuatilia ubora na viwango vya dawa zinazosambazwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati ufunguzi wa miradi hiyo ya PAVIA na PROFORMA, Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Profesa Muhammad Kambi amefafanua lengo ni kuweka mifumo ya kuthibiti ubora wa dawa barani Afrika.

Amesema miradi hiyo inafadhiliwa na programu ya maendeleo ya majaribio ya dawa kwa nchi za Ulaya na Afrika(EDCTP) na kusisitiza itasaidia pia kufuatilia kwa urahisi madhara ya dawa zinasambazwa na kutumiwa kwenye soko.

" Miradi hii itasaidia katika ufuatiliaji wa matukio baada ya mgonjwa kutumia dawa  husika , kubwa ni kuangalia imemsaidia kwa kiwango gani au imeleta madhara ili kuchukua hatua stahiki 
haraka,"amesema Profesa Kambi.

Ameongeza miradi hiyo kwa pamoja itashughulikia usalama wa  dawa kwa watumiaji na kubwa zaidi kudhibiti ubora wa dawa katika sehemu zote nchini na maeneo ya mipakani.Profesa Kambi ameongeza miradi hiyo inatarajiwa pia kuanza kwa kubuni mitaala maalum itakayotumiwa Vyuo Vikuu nchini ikiwa ni mkakati wa kuwandaa waafunzi mapema jinsi ya kukabiliana na matokeo ya dawa kwa mgonjwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Dawa  kutoka TFDA Adam Fimbo amesema usalama wa dawa nchini upo na mamlaka kupitia miradi hiyo miwili wataendelea kuboresha  huduma za upatikanaji na udhibiti wa dawa h afifu na bandia katika soko la dawa nchini . 

"Tumeungana na nchini kadhaa katika uanzishwaji na utekelezaji wa miradi hii katika harakati za kupambana matokeo baada ya mg onjwa kutumia dawa na kutengeneza mifumo inayoweza kuleta taarifa mapema na kuwasiliana kwa haraka na kubadilishana uzoefu,"amesema Fimbo.

Wakati huohuo Ofisa Mradi wa EDCTP Michelle Nderu amesema wameamua kufadhili miradi hiyo ili kuleta uzoefu kutoka nchi zilizoendelea na lengo ni kuboresha matumizi ya dawa sahihi kwa binadamu.
Mganga Mkuu wa Serikali- Wazara ya A f ya, P r of . M o ham mad B akar i Kambi, akiongea katika uzinduzi wa mi r adi mi ku bw a m iw il i ( P A V IA na PROFORMA) , inayolenga kuweka mi fu mo ya kut hi bi ti ub or a n a viwango vya madawa yanasambazwa n a ku tum iw a k atik a ma so ko ya Tanzania na nchi zingine za Afrika. ( P i ch a n a Mp i ga P ic ha W etu ) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...