Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
WAKALA wa Vipimo Tanzania(WMA) wamefanya ukaguzi wa tochi za Askari wa Usalama Barabarani katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kupima ubora wa vifaa hivyo vya usalama.
Ukaguzi huo umefanyika ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Vipimo duniani ambapo huadhimishwa kila ifikapo Mei 20 ya kila mwaka ambapo Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa amesema ukaguzi huo umelenga kupima ubora wa vifaa vya usalama barabarani ili kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa vyombo vya barabarani hapa nchini.
Pia amesema kumekuwepo malalamiko kwa watumiaji wa barabara kwa kuamini kuwa tochi zinazotumiwa na askari wa usalama barabarani zinawapunja speed, hivyo wameamua kuzipima ili kuangalia kama ni kweli ili kuondoa dhana iliyojengeka kwa tochi hizo.
Kwa upande wa Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai amewahimiza madereva kutii sheria bila shuruti ili kupunguza ajali barabarani.
Pia amewatoa hofu watumiaji wa barabarani kuwa tochi zinazotumiwa na askari wa usalama barabarani zimekaguliwa na hazina tatizo, hivyo ni kutii sheria na ukomo wa speed ili kupunguza ajali za barabarani.
Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) pamoja na Askari wa Usalama barabarani mkoani Pwani wakifanya vipimo vya ubora wa tochi za barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) Siraji Moyo(kushoto) pamoja na Glory Mtana (kulia) wakihakiki vipimo vinavyotolewa na tochi za barabarani ili kujilizisha wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa(kushoto) akielekezwa na mmoja wa Polisi wa usalama barabarani mkoani Pwani namna ya kupima spidi ya magari kwa kutumia tochi za Usalama barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya vipimo Duniani.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa tochi za Barabarani
zinazotumiwa Askari wa usalama Barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki
ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mrakibu
wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi –
Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akionesha mmoja ya
tochi wanazotumia askari wa usalama barabarani mara baada ya kufanyiwa
ukaguzi na Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) wakati wa maadhimisho ya wiki
ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mrakibu
Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Pwani
(ASP),Mossi Ndozero akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tochi
zilivyosaidia kupunguza ajali za barabarani ambapo mwaka huu zimepungua
sana mkoani humo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa, Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai, Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) pamoja na askari wa Usalama Barabari wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya ukaguzi wa tochi wanazotumia Askari wa Usalama Barabarani.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...