Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


KAMPENI ya ujenzi wa Choo cha Mtoto wa kike katika Halmashauri ya Manispaa jijini Dar es Salaam inakwenda vizuri kutokana na wadau walioahidi kuchangia kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa choo hicho kuendelea kutimiza ahadi zao zikiwamo za fedha ambapo Mratibu wa kampeni hiyo Tabu Shaibu amekabidhiwa Sh.milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo.

Akizungumza leo baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Shaibu ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini amesema ahadi zilizotolewa na wadau wa maendeleo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema zimeendelea kutekelezwa kwani wameendelea kupokea michango ya fedha na vifaa vya ujenzi kwa nyakati tofauti.

Amesema kampeni hiyo imetokana na uamuzi wa Watumishi Wanawake wa Manispaa hiyo uanzisha ujenzi wa choo hicho katika hivyo vitakavyojengwa kwenye shule za msingi na Shaibu amefafanua choo cha mfano kinajengwa Shule ya Msingi Chanika.Ujenzi umefikia hatua ya linta na kilichobaki ni kupaua.

"Tunashukuru kwa namna wadau mbalimbali wanavyoendelea kutimiza ahadi zao kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike.Tuendelee kusisitiza wale ambao bado hawajatimiza 
ahadi aidha ya fedha au vifaa vya ujenzi basi kuitekeleza."Lengo letu ni kutimiza lengo la kampeni hii ambayo tunakwenda kumkoamboa mtoto wa kike wa Manispaa ya Ilala ambaye leo yupo shuleni na siku zijazo atakuwa mtumishi wa manispaa yetu,"amesema Shaibu.

Kuhusu mchango wa Sh.milioni moja uliotolewa na Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa manispaa hiyo, Shaibu amesema anamshukuru kwa kutekeleza ahadi yake na hakika ameonesha dhamira njema ya kufanikisha ujenzi huo na kusisitiza amekuwa akipokea michango kwa nyakati tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali.

Kwa upande wa Mwaikambo amesema kikubwa ni kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike katika manispaa ya Ilala huku akisisitiza walioahidi watekeleze na kwamba ataendelea kushirikiana na watumishi wanawake na wadau wa maendeleo ili kampeni ifanikiwe."Niliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa choo hicho ambacho ni maalumu kwa mtoto wa kike.Hivyo nitaendelea kushirikiana na wadau wote kwa lengo la kufanikisha malengo yetu na wale ambao wameahidi niwaombe waendelee kutimiza ahadi zao,"amefafanua.

Wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mjema alisema ipo haja ya kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike na akifafanua vyoo kufafanua vyoo hivyo vitakuwa vya kisasa na ndani kutakuwa na mahitaji yote muhimu. 

 Mratibu wa Kampeni ya Ujenzi wa choo cha mtoto wa kike Tabu Shaibu ambaye pia Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati anapokea fedha Sh.milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo(kulia) kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo hicho.Kushoto ni Mhasibu wa Idara ya Elimu Msingi Manispaa hiyo Yasinta Endrew ya Ilala.

 Mratibu wa Kampeni ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike Tabu Shaibu ambaye pia Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam(kushoto) akipokea fedha Sh.milioni moja leo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo(kulia).Anayeshuhudia ni Mhasibu wa Idara ya Elimu Msingi Manispaa hiyo Yasinta Endrew ya Ilala .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...