Na Dixon Busagaga-MOSHI.

MWANAMKE aliyejifungua watoto Mapacha akiwa Mahabusu ,Marry Lukumay ameendelea kusota Gerezani na watoto wake baada ya kukosekana kwa wadhamini wenye sifa zinazokidhi masharti yaliyotolewa na Mahakama.

Miongoni mwa masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Hakimu mkazi ,Moshi ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro watakaosaini Fungu la Dhamana la kiasi cha sh laki tano kila mmoja.Marry Lukumay mkazi wa Babati mkoani Manyara kwa mara nyingine alifikishwa mahakama ya hakimu Mkazi ,Moshi baada ya kukamatwa Oktoba 15 mwaka jana kwa madai ya kukutwa na Mirungi kilogramu 10.

Katika shauri hilo namba 182 la mwaka 2017 ,mwendesha mashtaka upande wa Jamhuri ,Lilian Kowelo aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo kutokana na upelelezi kutokamilika .Hakimu anayesikiliza shauri hilo ,Pamela Meena alikubaliana na ombi hilo na kupanga June 27 mwaka huu ,mtuhumiwa kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo.

Akizungumza na mwanahabari wetu nje ya Mahakama ,Mwanamke huyo aliyewapa majina watoto wake ya Nora na Noreen wenye umri sasa wa miezi miwili sasa alisema alikamatwa mwaka jana katika eneo la Himo Oktoba mwaka jana.Alisema kuwa, Oktoba 24 Mwaka jana alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka linalomkabili na kuelezwa kuwa dhamana yake ipo wazi huku akitakiwa kuwa na wadhamini wawili.

Mary anayeshikiliwa katika Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro alisema wakati anakamatwa tayari alikuwa na ujauzito wa miezi miwili na Aprily 8 mwaka huu alijifungua watoto hao Mapacha katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...