Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Viongozi wa Jimbo hilo wataendelea kuwaunga mkono Wananchi wao hasa Vijana na Akina Mama walioamua kujituma katika muelekeo wa kujitafutia Maendeleo ili kujenga hatma njema ya maisha yao.
Alisema misaada ya kuyawezesha Makundi hayo katika kuyapatia vifaa, mtaji sambamba na maarifa itakuwa ikiendelea kila wakati kulingana na mahitaji halisi ya Wananchi ikilenga zaidi katika Vikundi vya Ushirika.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akikabidhi msaada wa Mashine iliyoitanguliwa na Boti ya kuvulia Samaki aliyoitoa kwa Kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Bahati Abeid Nassir kwa ajili ya Vijana wa Kikundi cha Hamasa cha Jimbo la Mahonda chenye Mastakimu yake Kijiji cha Fujoni hafla iliyofanyika Nyumbani kwake Kama Kaskazini kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema hakuna Tajiri au Kikundi cha Jamii kilichopata utajiri wa kushtukia bila ya kufanya kazi za ziada katika kujitafutia riziki ambazo Wanakikundi hao watalazimika kufanya jitihada zitakazowawezesha kujikwamua kutoka katika mazingira magumu ya maisha.
Balozi Seif aliwatahadharisha Wanachama wa Kikundi hicho cha Hamasa kwamba msaada huo wa Boti na Mshine yake usije geuka kuwa chanzo cha kuleta mifarakano baina yao.
Aliwataka Wanakikundi hao wapatao 50 walio jinsia mbili tofauti wafanye kazi kwa juhudi zao zote ili vifaa vya msaada waliopatiwa viwezeshe kuzaa vyengine kwa lengo la kutanua mradi wao unaopaswa kuwa wa kudumu.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akimkabidhi
Mashine ya Boti Katibu wa Kikundi cha Hamasisha cha Jimbo la Mahonda
Bibi Mwanapatima Othman Salum kwa ajili ya shughuli za Uvuvi za Kikundi
hicho. Kati kati yao ni Mkuu wa Nidhamu wa Kikundi cha Hamasa Bwana
Kichamu Haji Abdullah.
Mke
wa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Sul;eiman Iddi akitoa
nasaha kwa Wanachama wa Kikundi cha Hamasa mara baada ya kukabidhiwa
Mashine ya Boti hapo nyumbani kwae Kama.
Mkuu
wa Nidhamu wa Kikundi cha Hamasa Bwana Kichamu Haji Abdullah kwa niaba
ya wana kikundi wenzake akitoa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge wa
Jimbo la Mahonda kwa uamuzi wao wa kuwapatia Boti pamoja na Mashine
yake kwa ajili ya shughuli za Uvuvi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijumuika pamoja na
Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi yake katika futari ya pamoja
iliyofanyika kwenye Makaazi yake Kama.
Baadhi
na Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar wakijipatia vyakula kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud
Mohamed akitoa neon la shukrani mara baada ya futari ya pamoja
iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Seif. Picha na – OMPR – ZNZ.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...