Na Tiganya Vincent- Tabora
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi amepongeza hatua ya viongozi mbalimbali wa umma na sekta binafsi kwa kuandaa futari kwa kuwa jambo linasaidia kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Aggrey Mwanri.

Alisema ni kweli Serikali haina dini lakini wananchi wanazo dini na hivyo hatua hiyo inaoonyesha mapenzi makubwa waliyonayo kwa watu wote bila kujali tofauti zao , hali inayosaidia kuimarisha umoja wa Kitaifa ulioasisiwa tangu uhuru wa Nchi ya Tanzania.

Sheikh Mavumbi aliwataka watu wengine ambao Mwenyezi Mungu amejalia kuwa na uwezo wa kifedha kuigia mfano ulionesha na baadhi ya viongozi wakiwemo wa Kitaifa wa kutoa futari kwa watu bila kujali rika na uwezo wao aua hali zao za kimaisha.

Aidha Sheikh huyo wa Mkoa aliwaomba umma wa kiislamu katika Mkoa wa Tabora endapo watafanikiwa kuuona mwezi muandamo kushiriki Swala ya eid El fitri itakayoswaliwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ikiwa ni baada ya kukamilika mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) akisalimia na Sheikh wa Mkoa wa Tabora wa Ahamadiyya  Musilim Jamaat Tanzania  Shafi Mohamed Memon (kulia) jana mjini hapa wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za Mkoa mara baada ya kufuturisha jana mjini hapa. 
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi akitoa salamu za Waislamu wa Mkoa huu baada ya futari iliyoandaliwa  jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Aggrey Mwanri.
 Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini na Serikali walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakifuatilia hotuba ya Sheikh wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi(hayupo katika picha)
  Baadhi ya Viongozi wa dini walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...